1
سم لله الرحمن الرحيم WAJUMBE WA JOPO LA MASHEIKH MCHAKATO WA MAHAKAMAA
YA KADHI Kumb. Na WJM/BKT/01/2012 29 Shaaban, 1433 17 Julai, 2012 Kwa:
Mufti Sheikh Issa bin Shaaban, MUFTI WA BAKWATA, S.L.P DAR ES SALAAM.
لیكم و رحمة لله, السلام YAH: KWENDA KINYUME NA JOPO LA MASHEIKH
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu. Sisi masheikh
tulioorodhesha majina yetu hapa chini, ambao ni wajumbe katika Jopo la
Msheikh 25 wa taasisi na jumuiya mbali mbali zilizosajiliwa kisheria
ambalo tangu liundwe limekuwa katika mazungumzo na serikali kuhusu suala
la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini, tumepokea habari kwamba
umeteua Kadhi Mkuu, manaibu wake wawili na makadhi wa mikoa kwa mshangao
mkubwa na tungependa ufahamu kwamba. Mosi, maamuzi yako ya
kuteua makadhi wakati suala hili lilikuwa bado halijafikia hitimisho, ni
maamuzi batili kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, hadidu rejea za
Jopo, sheria za nchi na pia hata uhalisia wa mambo tu ulivyo kuhusu
suala hili. Pili, maamuzi yako yamemfanya Waziri Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aonekane si mkweli kwa
sababu kwa muda wote wa miaka miwili amekuwa akimfamhamisha Mhe.
Rais, wabunge, waislamu na watanzania kwa ujumla kwamba kuna mazungumzo
kati ya kamati ya masheikh na serikali na mara ya mwisho kikao cha
kamati hiyo na Waziri Mkuu kilifikia hatua ambazo utekelezaji wake ndio
ungetoa picha waislamu wanaanzishaje Mahakama ya Kadhi nchini.
2 Tatu, Kadhi Mkuu na Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya
Kadhi tunayoipigania muda wote huu kwa sababu bado Mahakama ya Kadhi
haijaundwa kwa mujibu wa makubaliano ya kikao chetu cha mwisho na Waziri
Mkuu na pia ki-Shariah na ki-Sheria hauna mamlaka ya kuwateulia
waislamu wote nchini makadhi. Kutokana na mas’ala hayo matatu
tuliyoyataja hapo juu, tunataka ufanye yafuatayo kwa maslahi ya
Uislamu;- i) Utangaze kwamba umekosea kwa kukiuka mojawapo ya
hadidu rejea za jopo na kwamba Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama
ya Kadhi ambayo waislamu tunaipigania kwa muda wa miaka kadhaa sasa na
ambayo Jopo la Masheikh tulikubaliana tangu mwanzo wa mchakato huu wa
Mahakama ya Kadhi baina ya waislamu na serikali na uainishe kwamba hao
ni makadhi wa Bakwata na si makadhi wa waislamu wote. ii)
Uwauzulu mara moja makadhi wote uliowatangaza kwa maamuzi yako binafsi
pasina kuwashirikisha masheikh wote wa Jopo la Masheikh 25 ambalo ndilo
linalotambulika na serikali kuwakilisha waislamu wote nchini. Kwa mujibu
wa hadidu rejea, tulikubaliana kwamba “mtu yeyote katika jopo la
Masheikh 25 hapaswi kusema lolote lile ambalo halina maamuzi ya pamoja
ya wajumbe wa Jopo”. iii) Uitishe kikao cha haraka cha Jopo
la Masheikh 25 ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya kupokea barua hii
vinginevyo tutautangazia ummah kwamba hatuna imani na wewe kuongoza
mchakato huu na tutachukua hatua stahiki kukabiliana na udikteta huu.
iv) Kwa kuwa umeonesha kutoa maamuzi ya kidikteta, katika kikao cha
kwanza tu cha Jopo la masheikh 25 kitakachoitishwa ndani ya wiki moja
tuliyoitaja hapo juu, kitachagua Makamu M/Kiti, Naibu Katiba na
kuhakikisha kwamba ummah wa waislamu nchini unahusishwa ikiwa ni pamoja
na kupanua wigo wa taasisi zitakazoshiriki katika kadhia hii ya Mahakama
ya Kadhi. 3 Wabillahi Tawfiiq, Signed M/Kiti wa Kamati Ndogo
ya Jopo la Masheikh WAJUMBE WAFUATAO WAMESAINI KUUNGA MKONO MSIMAMO HUU
Names and signatures omitted on purpose Nakala kwa: 1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu, Dar es Salaam.
2. Waziri Mkuu, Ofisi ya waziri Mkuu, Ikulu, Dar es Salaam. 3. Spika wa Bunge, Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam. 4. Waziri wa Katiba na Sheria Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam. 5. Mwanasheria Mkuun wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Dar es Salaam. 6. Mhe Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania. 7. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dar es Salaam. 8. Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu Tanzania |
No comments:
Post a Comment