Wednesday, December 12, 2012

TIGO YAUNGA MKONO MAADHIMISHO YA MIAKA 15 YA FM ACADEMIA



Kampuni ya Simu za Mkononi Tigo imeamua kuwapiga Tafu Bendi  maarufu nchini Tanzania FM academia katika Sherehe yao ya kutimiza miaka 15.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Tigo Bw, Alex Msigara amesema kuwa Tigo itatuma ujumbe mfupi kwa wateja wake wote  wa jiji la Dar es Salaam kuwapa Taarifa  juu ya Maadhimisho ya  miaka 15 ya Bendi ya FM ACADEMIA  yatakayofanyika tarehe 14 Desemba mwaka huu katika  New Msasani each jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.

Kwa Upande wao FM AKADEMIA wamesema kuwa wamefurahi  kwa kuwezeshwa na Tigo katrika sherehe yao ya kusherekea kutimiza miaka 15 tangu kutimizwa kwa Bendi hiyo.
Afisa Matukio wa FM Academia  Bw, Nassib Mahunya  amesema kuwa katika sherehe hiyo Keki itakatwa na watafunguaq Shampein ambapo watasindikizwa na Bendi ya Mapacha watatu ambayo itatoa burudani siku hiyo.
Picha hizo zinawaonyesha wasanii wa Bendi hiyo walipokuwa katika Mkutano wa waandishi wa Habari ulioandaliwa na Tigo.

No comments:

Post a Comment