Friday, December 14, 2012

Chuo cha Mafunzo Eagle Wing Chaadhimisha Miaka Mitano Pamoja na Watoto Yatima

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=72a8d77bb8&view=att&th=13b99c8235106539&attid=0.3&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P_55BzOQSmT9ZMqhrg9kiHp&sadet=1355510838699&sads=i0EXjval3Rf2g4X8NOEpTAEa4q0  

Mkurugenzi Mkuu wa Chuo Cha Eagle Wing Akikabidhi Zawadi Kwa Sister In charge wa kituo hicho wakati Uongozi na Wanafunzi wa Eagle Wing walipotembelea Kituo hicho ikiwa ni moja ya maadhimisho yao ya Miaka mitano{5} tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.


Chuo cha Mafunzo Eagle Wing kimetimiza Miaka Mitano tangu kuanzaishwa kwake Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa maadhimisho ya Miaka Mitano tangu kuanzishwa kwa Chuo Hicho mwaka 2007 Mkurugenzi Mkuu wa Eagle Wing Bw Samwel Sinda Amesema chuo chake kimepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya Udahili wa Wanafunzi Chuoni hapo kwani walianza na Wanafunzi wa Nne wakat chuo kinaanza ila sasa udahili wa Wanafunzi umeongezeka na kufika Mia tano lakini licha ya mafanikio ambayo Chuo imeyapata ndani ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake chuo hicho kinakabiriwa na changamoto kubwa ya wanafunzi wengi katika Chuo hicho kushindwa kulipa ada Kwa wakati na wengine kushindwa kulipa Ada kabisa kutokana na uwezo wao wa kifedha kuwa mdogo ambapo katika Hotuba yake kwa Mageni Rasmi katika Maadhimisho hayo Bw: David Kazuva Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi Stadi wizara ya elimu kwa niaba ya waziri wa Elimu na Ufundi Stadi Mh: Dr Sukuru Kawambwa  mkurugenzi huyo wa chuo alimuomba Mgeni Rasmi kufikisha Kilio hicho kwa wahusika ili wapate luzuku hata ikiwezekana utengenezwe utaratibu wa kutoa mikopo kwa Vyuo vyote vinavyotoa Elimu chini ya usimamizi wa Veta ili Kuwapunguzia mzigo wanafunzi wasiojiweza kifedha kwani wahitaji ni wengi katika vyuo hivyo. 
Maadhimisho hayo yameenda Sanjal na utowaji wa zawadi kwa watoto yatima katika kituo cha msimbazi center kinachotoa huduma hizo chini ya uongozi wa Kanisa Katoriki jimbo kuu la Dar es salaam ambapo Sister In charge wa kituo hicho ameushukuru uongozi wa chuo hicho hasa Mkurugenzi Bwana Sinda Kwa Kutambua umuhimu wa Wa watoto hao na kuwajali ambapo amezitaka Taasis nyingine kuiga mfano wa  Eagle Wing Kutumia faida wanazozipata katika Biashara zao kuwasaidia Watu wenye uhitaji kama Watoto hao wa Msimbazi Center Jijini Dar Es Salaam


https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=72a8d77bb8&view=att&th=13b99c8235106539&attid=0.1&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P_55BzOQSmT9ZMqhrg9kiHp&sadet=1355510831245&sads=331Ea4vuMD39B8zZQzsyop1HWXQ  
Baadhi ya Wanafunzi ,Uongozi Wa eagle Wing wakiwa kenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Center mara Baada ya kukabidhiwa zawadi kutoka Eagle Wing.
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=72a8d77bb8&view=att&th=13b99c8235106539&attid=0.4&disp=inline&safe=1&zw&saduie=AG9B_P_55BzOQSmT9ZMqhrg9kiHp&sadet=1355510841793&sads=5GGEdeRJHq63HBuaLk3xeRYsJ7U 

 Wanafunzi Waliokuwa katika Maandamano kuelekea katika Viwanja vya Shule ya Secondary ya Mkapa ambapo kilele cha maadhimisho hayo yalifanyika Rasmi.

No comments:

Post a Comment