Naibu Mkurugenzi mkuu wa T.B.S Mh: Leandri Kinabo akiongea na Waandishi
wa Habari mara baada ya Kukabidhi Leseni kwa Makampuni mbalimbali ya
biashara amabapo nae alisema kuwa "pamoja na chanagamoto mbalimbali
zinazo ikabili T.B.S ila bado shirika hili linajitahidi kutoa huduma
zilizobora na kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata Bidhaa zilizobora na
Viwango stahiki aidha ametoa wito kwa makampuni mbalimbali ambayo jana
yalikabidhiwa rasmi leseni zao kuwa watengeneze bidhaa zenye ubora wa
kimataifa ili kuhimili Soko la ndani na Nje ya nchi na kuleta ushindani
kwa makampuni mengine ya Afrika na nje ya Afrika.
Katibu Mkuu wa Shirika la Viwango la kimataifa (I.S.O) Mh: Rob Steele akiongea mara baada ya kukabidhi Leseni kwa makampuni takribani 19 ambapo ametoa wito kwa Makampuni hayo kuiunga mkono T.B.S kwani kudhalisha kwao bidhaa zilizo bora zitaongeza sifa na ufanisi kwa T.B.S kwani Wadau Mbalimbali watadhidi kujenga imani kwa shrika hilo.
Mh: Rob Steele Akimkabidhi Leseni ya viwango vya Ubora na Biashara Mkurugenzi wa Kampuni Ya Maji (Mamas Fresh Water) Mama Salama Salmin Amour Jana Katika hafra fupi ya kukabidhi leseni hizo kwa Makampuni 19 Ya Biashara. Ambapo leseni hizo zilitolewa na Katibu mkuu wa shirika la Viwango La Kimataifa ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika hafra hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni Ya Maji (Mamas Fresh Water) Mama Salama Salmin Amour Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya Kukabidhiwa Leseni ya biashara kutoka shirika la viwango Tanzania {T.B.S} ambapo ameshukuru T.BS kwakumpatia leseni hiyo kwa uharaka zaidi bila Mizengwe nakuahaidi kampuni yake kuzalisha Bidhaa zenye ubora na kiwango cha Hali ya juu kulingana na Hadhi ya Leseni aliyopewa na T.BS. aidha aliongeaza kuwa kampuni yake licha ya kutngeneza maji amabayo yanapatikana kwa ujazo wa juu kwa Lita 20 Na ujazo wa chini Nusu Lita kampuni yake pia Inauza Chupa Tupu za maji Loshen pamoja na Nembo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni Ya Mama`s Fresh Water {Mbele} wakiwa kwenye Hafra hiyo.
No comments:
Post a Comment