IKIWA
kesho kutwa (Juni 16) ndio pazia la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS)
linafunguliwa rasmi kwa kuanza kutafuta vipaji mkoani Dodoma ambapo maelfu ya watu wameonesha nia ya kujitokeza kushiriki.
Mkoani
hapa vijana wengi wameonesha kuwa na shauku kubwa ya kusubiria
kushiriki katika usaili huo ambapo unaanza rasmi keshokutwa (Jumamosi ya
Juni 16) katika ukumbi wa Royal Village.
Shauku
hiyo inaweza kuwa inasababishwa na dau la zawadi la milioni 50
lililotangazwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel lakini pia dili
la kuendelezwa kisanii ambalo nalo linawavutia vijana zaidi.
Akizungumzia
usaili wa kesho kutwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampun ya Benchmark
Production Ritha Paulsen alisema kuwa usaili wa mwaka huu watachukua
washiriki kuanzia miaka 16 na kuendelea.
Alisema kuwa uamuzi huo wa kuchukua
washiriki wa kuanzia miaka 16 ni kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa
kuimba na kupanga sauti ili nao wajaribu bahati yao.
“Najua
kwa mwaka huu kwa kuwa shindano hili linadhaminiwa na Zantel hivyo
mambo yamekuwa ni makubwa zaidi na napenda kuwaomba vijana kujitokeza
kwa wingi zaidi kutumia fursa hii ambayo Zantel inawapatia mwaka huu”
alisema Ritha.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Ali
Bin Jarsh akizungumzia shindano hilo alisema kuwa Zantel inatambua
nafasi ya muziki katika kukuza ajira na nchini.
Alisema
kuwa Zantel imeamua kupitia Epiq Bongo Star Search kuinua vipaji vya
vijana katika muziki ikiwa pamoja na kuwatengenezea njia ya mafaniko.
No comments:
Post a Comment