Wednesday, December 19, 2012

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KATA YA KIPAWA WAPATA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA UJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga akifungua Mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Kushoto ni Msaidizi wa Waziri Mohamed Michuzi, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa Said Fundi na Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa.
Wakina mama wajasiriamali wakiwa katika mafunzo hayo
Wanawake Wajasiriamali wakisubiri  kuingia katika mafunzo hayo


Na Dotto Mwaibale

NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga amesema ukosefu wa ajira hapa nchini ni jambo tete ambapo kila mtu anatakiwa kujiajiri mwenyewe ili kukabiliana na sua hilo.

Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake wa Kata ya Kipawa Dar es Salaam leo.

Alisema suala la upatikanaji wa ajiri haipaswi kuachiwa kwa serikali pekee bali kila mtu mmoja mmoja alipo anatakiwa kupambana na suala hilo kwa kujiajiri kama wanavvyo fanya wanawake hao wa Kata ya Kipawa.

“Kazi ya Serikali ni kuhakikisha inawapunguzia mzigo wananchi kwa kujenga Zahanati, Madarasa, barabara na si kuwanunulia chakula wananchi ambao ni wajibu wao” alisema  Dk.Mahanga.

Alisema suala la ajira linachangamoto kubwa si kwa Tanzania bali dunia nzima isipo kuwa linatofautiana kimazingira kwani kwa nchi zilizoendelea wanapo sema hawana ajira  ni katika sekta za viwanda, serikali na katika sekta rasmi tofauti na hapa kwetu.

Alisema kwa hapa nchini suala hili ni tete kwa sababu hatuna viwanda vya kutosha na ajira zinazotolewa serikali ni chache hivyo njia pekee ya kujikwamua ni kujiajiri wenyewe kwa kujiingiza katika ujasiriamali.

Dk. Mahanga alitumia fursa hiyo kuwapongeza akina mama hao kwa kuzarisha ajira 300 ambapo kama kila mmoja katika eneo lake la kazi atakuwa na watu wawili anaofanya nao kazi watakuwa na jumla ya watu wenye ajira 600.

Aliwataka wanawake hao kutumia mafunzo hayo kwa kuendelea kufanyakazi kwa bidii na kuwataka vijana kuiga njia hiyo na kujiajiri badala ya kucheza ‘pool’ kutwa nzima huku wakiilalamika serikali kuwa haitoi ajira.

Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa alisema semina hiyo imejumuisha wanawake 300 kutoka katika eneo hilo na kuwa semina nyingine kama hiyo itafanyika mwakani mwezi februari na mafunzo hayo yamedhaminiwa na Benki ya Equity na Darling Hair.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa kata hiyo ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali wakati wakifanya biashara zao na kuinua kipato chao  na kuwa ukimuinua kiuchumi mwanamke unakuwa umeliinua taifa zima.

MSANII SAJUKI AANGUKA JUKWAANI MKOANI ARUSHA

Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
Msanii huyo akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole.
Msanii wa filamu nchini,Juma Kilowoko akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafai ya kuwasalimia mashabiki wake
(Picha na mdau wa Fullshangwe Mahmoud Ahmad-Arusha)
………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad,Arusha
 
HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
 
Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
 
Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
 
Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.
 
Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
 
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
 Hatahivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.
 
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.
 
“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba

TIGO YACHEZESHA DROO YA WASHINDI WA MWISHO WA MWAKA

Meneja Internet wa Tigo Bw, Titos Kafuma akizungumza na waandishi wa Habari leo  katika Hoteliya Southern Sun juu ya Uchaguzi wa washindi wa Mwisho wa Mwaka wa Droo ya Snmart card na  Ascend  Y200.Ambapo Tigo imefanikiwa kuchagua washindi kumi wa Droo ya ya Smartcard leo na kufanya jumla ya washindi kufikia 94.
 Amesema kuwa Droo hizo  zimeshuhudiwa na kuendeshwa na Bodi ya Taifa ya Bahati nasibu kwakutumia Compyuta ambayo itachagua washindi kwa kutumia mpangilio usio maalum.

Mshindi wa Kwanza leo katika Droohiyo amefanikiwa kujishindia TV aina ya Samsung ya nchi 30 ambaye anafahamika kwa jina la Judy Kesy Mkazi wa Dar es Salaam ambapowengine watajipatia Simu kutoka Tigo.
David Semkwao ambaye ni Mbunifu wa Ofa za Internet za Tigo wakwanza kutoka kushoto pamoja na Maofisa wengine wa Tigo wakichezesha Droo iliyofanikiwa kumpata mshindi wa Kwanza kutoka  Dar es Salaam.

Monday, December 17, 2012

DK. SHEIN AENDELEZA MIKUTANO NA WIZARA MBALIMBALI, LEO AKUTANA NA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya  Nchi Ofisi ya Rais, ,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
Watendaji katika Wizara ya Nchi  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,wakiwa katika Mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika utekelezaji wa kazi za  Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Mwadini Makame,(kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Wizara hiyo,katika Mkutano  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ukujumuisha na watendaji  katika ukumbi wa Mkutano wa Ikulu Mjini Zanzibar,ikiwa ni mfululizo kwa kila Wizara kuzungumzia  utekelezaji wa kazi zake.

WAISLAMU WANAHOJI BAADA YA BARUA HII KWA MUFTI SIMBA KUNANINI KINAENDELEA? Kama majibu yapo yatume wahusika wanataka majibu!


1 سم لله الرحمن الرحيم WAJUMBE WA JOPO LA MASHEIKH MCHAKATO WA MAHAKAMAA YA KADHI Kumb. Na WJM/BKT/01/2012 29 Shaaban, 1433 17 Julai, 2012 Kwa: Mufti Sheikh Issa bin Shaaban, MUFTI WA BAKWATA, S.L.P DAR ES SALAAM. لیكم و رحمة لله, السلام

YAH: KWENDA KINYUME NA JOPO LA MASHEIKH
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu. Sisi masheikh tulioorodhesha majina yetu hapa chini, ambao ni wajumbe katika Jopo la Msheikh 25 wa taasisi na jumuiya mbali mbali zilizosajiliwa kisheria ambalo tangu liundwe limekuwa katika mazungumzo na serikali kuhusu suala la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini, tumepokea habari kwamba umeteua Kadhi Mkuu, manaibu wake wawili na makadhi wa mikoa kwa mshangao mkubwa na tungependa ufahamu kwamba.

Mosi, maamuzi yako ya kuteua makadhi wakati suala hili lilikuwa bado halijafikia hitimisho, ni maamuzi batili kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, hadidu rejea za Jopo, sheria za nchi na pia hata uhalisia wa mambo tu ulivyo kuhusu suala hili.

Pili, maamuzi yako yamemfanya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aonekane si mkweli kwa sababu kwa muda wote wa miaka miwili amekuwa akimfamhamisha Mhe.

Rais, wabunge, waislamu na watanzania kwa ujumla kwamba kuna mazungumzo kati ya kamati ya masheikh na serikali na mara ya mwisho kikao cha kamati hiyo na Waziri Mkuu kilifikia hatua ambazo utekelezaji wake ndio ungetoa picha waislamu wanaanzishaje Mahakama ya Kadhi nchini.

2 Tatu, Kadhi Mkuu na Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya Kadhi tunayoipigania muda wote huu kwa sababu bado Mahakama ya Kadhi haijaundwa kwa mujibu wa makubaliano ya kikao chetu cha mwisho na Waziri Mkuu na pia ki-Shariah na ki-Sheria hauna mamlaka ya kuwateulia waislamu wote nchini makadhi. Kutokana na mas’ala hayo matatu tuliyoyataja hapo juu, tunataka ufanye yafuatayo kwa maslahi ya Uislamu;-

i) Utangaze kwamba umekosea kwa kukiuka mojawapo ya hadidu rejea za jopo na kwamba Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya Kadhi ambayo waislamu tunaipigania kwa muda wa miaka kadhaa sasa na ambayo Jopo la Masheikh tulikubaliana tangu mwanzo wa mchakato huu wa Mahakama ya Kadhi baina ya waislamu na serikali na uainishe kwamba hao ni makadhi wa Bakwata na si makadhi wa waislamu wote.

ii) Uwauzulu mara moja makadhi wote uliowatangaza kwa maamuzi yako binafsi pasina kuwashirikisha masheikh wote wa Jopo la Masheikh 25 ambalo ndilo linalotambulika na serikali kuwakilisha waislamu wote nchini. Kwa mujibu wa hadidu rejea, tulikubaliana kwamba “mtu yeyote katika jopo la Masheikh 25 hapaswi kusema lolote lile ambalo halina maamuzi ya pamoja ya wajumbe wa Jopo”.

iii) Uitishe kikao cha haraka cha Jopo la Masheikh 25 ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya kupokea barua hii vinginevyo tutautangazia ummah kwamba hatuna imani na wewe kuongoza mchakato huu na tutachukua hatua stahiki kukabiliana na udikteta huu.

iv) Kwa kuwa umeonesha kutoa maamuzi ya kidikteta, katika kikao cha kwanza tu cha Jopo la masheikh 25 kitakachoitishwa ndani ya wiki moja tuliyoitaja hapo juu, kitachagua Makamu M/Kiti, Naibu Katiba na kuhakikisha kwamba ummah wa waislamu nchini unahusishwa ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa taasisi zitakazoshiriki katika kadhia hii ya Mahakama ya Kadhi.

3 Wabillahi Tawfiiq, Signed M/Kiti wa Kamati Ndogo ya Jopo la Masheikh WAJUMBE WAFUATAO WAMESAINI KUUNGA MKONO MSIMAMO HUU Names and signatures omitted on purpose Nakala kwa:

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu, Dar es Salaam.

2. Waziri Mkuu, Ofisi ya waziri Mkuu, Ikulu, Dar es Salaam.

3. Spika wa Bunge, Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam.

4. Waziri wa Katiba na Sheria Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam.

5. Mwanasheria Mkuun wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Dar es Salaam.

6. Mhe Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

7. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dar es Salaam.

8. Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu Tanzania

TIGO NA MAMBO MAPYA


Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Tigo Goodluck Charles, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu huduma mpya inayomuwezesha mteja kununua kifurushi cha Extreme kupitia Tigopesa, kushoto ni Afisa Masoko wa Tigo Jacqeline Nnunduma na Afisa Uhusiano wa Tigo Mariam Mlangwa.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wakitangaza huduma mpya ya kununua kifurushi cha Xtreme kupitia Tigopesa.
FAIDA atakazopata mteja atakayetumia huduma ya Xtreme kupitia tigopesa ni pamoja na muda wa nyongeza wa Tsh.450 utakao muwezesha kupiga simu kwenda mitandao yote nchini. Mbali na hilo wateja wataweza kununua vifurushi hivyo kwaajili ya ndugu jamaa na marafiki.

BODI ZA MFUKO WA BARABARA NA WAKALA WA BARABARA ZA ZINDULIWA JIJINI DAR LEO.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akimpa zawadi Mjumbe wa Bodi ya mfuko wa Barabara aliemaliza muda wake kwa mujibu wa sheria za Bodi Mhandisi Omar Chambo (kushoto) ,Waziri Magufuli amemshukuru Mhandisi Omar Chambo. ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na wajumbe wengine waliomaliza muda wao kwa mchango mkubwa walioutoa katika mfukona kuleta ufanisi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza wakati akizindua Bodi ya Mfuko wa Barabara na Bodi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) leo jijini dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hizo leo jijini Dar es salaam , ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Bodi ya ya Mfuko wa Barabara Dr. James Wanyancha akitoa hotoba yake wakati wa uz