Monday, December 17, 2012

WAISLAMU WANAHOJI BAADA YA BARUA HII KWA MUFTI SIMBA KUNANINI KINAENDELEA? Kama majibu yapo yatume wahusika wanataka majibu!


1 سم لله الرحمن الرحيم WAJUMBE WA JOPO LA MASHEIKH MCHAKATO WA MAHAKAMAA YA KADHI Kumb. Na WJM/BKT/01/2012 29 Shaaban, 1433 17 Julai, 2012 Kwa: Mufti Sheikh Issa bin Shaaban, MUFTI WA BAKWATA, S.L.P DAR ES SALAAM. لیكم و رحمة لله, السلام

YAH: KWENDA KINYUME NA JOPO LA MASHEIKH
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu. Sisi masheikh tulioorodhesha majina yetu hapa chini, ambao ni wajumbe katika Jopo la Msheikh 25 wa taasisi na jumuiya mbali mbali zilizosajiliwa kisheria ambalo tangu liundwe limekuwa katika mazungumzo na serikali kuhusu suala la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini, tumepokea habari kwamba umeteua Kadhi Mkuu, manaibu wake wawili na makadhi wa mikoa kwa mshangao mkubwa na tungependa ufahamu kwamba.

Mosi, maamuzi yako ya kuteua makadhi wakati suala hili lilikuwa bado halijafikia hitimisho, ni maamuzi batili kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, hadidu rejea za Jopo, sheria za nchi na pia hata uhalisia wa mambo tu ulivyo kuhusu suala hili.

Pili, maamuzi yako yamemfanya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aonekane si mkweli kwa sababu kwa muda wote wa miaka miwili amekuwa akimfamhamisha Mhe.

Rais, wabunge, waislamu na watanzania kwa ujumla kwamba kuna mazungumzo kati ya kamati ya masheikh na serikali na mara ya mwisho kikao cha kamati hiyo na Waziri Mkuu kilifikia hatua ambazo utekelezaji wake ndio ungetoa picha waislamu wanaanzishaje Mahakama ya Kadhi nchini.

2 Tatu, Kadhi Mkuu na Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya Kadhi tunayoipigania muda wote huu kwa sababu bado Mahakama ya Kadhi haijaundwa kwa mujibu wa makubaliano ya kikao chetu cha mwisho na Waziri Mkuu na pia ki-Shariah na ki-Sheria hauna mamlaka ya kuwateulia waislamu wote nchini makadhi. Kutokana na mas’ala hayo matatu tuliyoyataja hapo juu, tunataka ufanye yafuatayo kwa maslahi ya Uislamu;-

i) Utangaze kwamba umekosea kwa kukiuka mojawapo ya hadidu rejea za jopo na kwamba Makadhi uliowateua si makadhi wa Mahakama ya Kadhi ambayo waislamu tunaipigania kwa muda wa miaka kadhaa sasa na ambayo Jopo la Masheikh tulikubaliana tangu mwanzo wa mchakato huu wa Mahakama ya Kadhi baina ya waislamu na serikali na uainishe kwamba hao ni makadhi wa Bakwata na si makadhi wa waislamu wote.

ii) Uwauzulu mara moja makadhi wote uliowatangaza kwa maamuzi yako binafsi pasina kuwashirikisha masheikh wote wa Jopo la Masheikh 25 ambalo ndilo linalotambulika na serikali kuwakilisha waislamu wote nchini. Kwa mujibu wa hadidu rejea, tulikubaliana kwamba “mtu yeyote katika jopo la Masheikh 25 hapaswi kusema lolote lile ambalo halina maamuzi ya pamoja ya wajumbe wa Jopo”.

iii) Uitishe kikao cha haraka cha Jopo la Masheikh 25 ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya kupokea barua hii vinginevyo tutautangazia ummah kwamba hatuna imani na wewe kuongoza mchakato huu na tutachukua hatua stahiki kukabiliana na udikteta huu.

iv) Kwa kuwa umeonesha kutoa maamuzi ya kidikteta, katika kikao cha kwanza tu cha Jopo la masheikh 25 kitakachoitishwa ndani ya wiki moja tuliyoitaja hapo juu, kitachagua Makamu M/Kiti, Naibu Katiba na kuhakikisha kwamba ummah wa waislamu nchini unahusishwa ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa taasisi zitakazoshiriki katika kadhia hii ya Mahakama ya Kadhi.

3 Wabillahi Tawfiiq, Signed M/Kiti wa Kamati Ndogo ya Jopo la Masheikh WAJUMBE WAFUATAO WAMESAINI KUUNGA MKONO MSIMAMO HUU Names and signatures omitted on purpose Nakala kwa:

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu, Dar es Salaam.

2. Waziri Mkuu, Ofisi ya waziri Mkuu, Ikulu, Dar es Salaam.

3. Spika wa Bunge, Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam.

4. Waziri wa Katiba na Sheria Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam.

5. Mwanasheria Mkuun wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Dar es Salaam.

6. Mhe Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

7. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Dar es Salaam.

8. Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu Tanzania

No comments:

Post a Comment