Shujaa aliyekuwa hategemewi,
mjerumani, ambaye sasa ana miaka 73, akawa mungu wa soka nchini Ugiriki
baada ya kuiongoza nchi hiyo kwenye kubeba kombe mwaka 2004
Akiwa bingwa wa kuunda ukuta wa kupaki basi golini chini ya nahodha,
Theo Zagorakis kutoka Leicester City, Rehhagel alifanya maajabu mwaka
2004.
Aliiongoza timu yake kupita kwenye hatua ya makundi huku wakishinda
mechi zote kwa ushindi wa 1-0 - hata ushindi wa fainali dhidi ya Ureno
ulikuwa wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji.
Siri ya mafanikio? Nyuma ya kila kocha aliyefanikiwa kuna mke mzuri wa
kocha huyo na mama watoto wa Otto, Beate, ameripotiwa huwa anaenda
kufanya scouting kwa wapinzani kwa ajili ya mumewe. |
No comments:
Post a Comment