Kocha
Kim Poulsen ametaja kikosi cha Taifa Stars ambacho leo (Juni 2 mwaka
huu) kitakuwa uwanjani kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini
Abidjan kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Amefanya
mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu
kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu.
Amir
Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho
Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza
nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia
mazoezini siku moja kabla ya safari.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
Wachezaji wa akiba;
Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon
Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim
amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na
kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika
90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2
kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)
No comments:
Post a Comment