Thursday, June 28, 2012

YALIYOJIRI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI JANA

Yaliotokea jana katika hospitali ya taifa Muhimbili baada ya askali wa upelelezi alipojikuta anaambuli kipigo kutoka kwa watu waliokuwepo kwa ajili ya kumuangalia Mwenyekiti wa jumuhiya ya madaktari inayeongoza mgomo wa madaktari Dr,Steven Ulimboka aliepigwa na watu wasiojulikana  na kujeruhiwa vibaya.

Hata hivyo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jana alionya juu ya wananchi kuchukua hatua mikononi bila kufuata sheria kwa  kuwa zinaweza kuleta madhara hata kwa ndugu zao kwani kachelo huyo alikuwa kazini  na ndiye aliyefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa suala la  Dk. Steven Ulimboka linashughulikiwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuletwa hospitali

No comments:

Post a Comment