Kiingilio
cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia itakayochezwa Jumamosi (Juni
17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 2,000.
Kiwango
hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani na rangi ya chungwa.
Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 48,590 kwenye
uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Viingilio
vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000 kwa
VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani
siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
No comments:
Post a Comment