Wednesday, May 23, 2012

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA YASITISHA KWA MUDA UZINDUZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Bw.Dickson Maimu Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi leo makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa jijini Dar es salaam kuhusu kusitishwa kwa muda uzinduzi wautoaji vitambulisho vyaya Taifa uliokuwa ufanyike mapema mwezi huu ili kupisha kuyafanyia kazi mapendekezo ya wadau ili yaweze kuingia kwenye mfumo.hata ivyo Bw.Dickson Maimu amesema mradi umekamilika ila zimejitokeza changamoto na maitaji ya msingi kutoka kwa wadau muhimu wa vitambulisho vya Taifa kwa hiyo mamlaka haina budi kuyafanyia kazi ili kitambulisho kiwe kimekidhi maitaji yote yamsingi.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo leo katika makao makuu ya mamlaka ya vitambulisho vya taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment