Thursday, December 6, 2012

WATANZANIA WATAKIWA KUHAMIA KWENYE MFUMO WA DIGITALI KUFIKIA TAREHE 31 MWEZI HUU AMBAPO MFUMO WA ANALOGIA UTAFUNGWA

Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof, Makame Mbalawa akionyesha moja ya Televisheni inayotumia mfumo wa Digitali baada ya kuondokana na Analogia mbele ya waandishi wa habari katika mkutano mkuu wa watangazaji wa mwaka uliofanyika leo katika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
 ...................................................................................................................
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof Mbalawa amewataka watanzania kuichangamkia huduma ya Digitali haraka iwezekanavyo ili kuepukana na nchi nyingine kuifanya Tanzania Dampo la kutupia vitu vya Analogia.
Akizungumza katika Hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal amewataka wamiliki wa Vyombo vya habari kutengeneza vipindi vinavyotoa mwanya kwa habari za maendeleo ya wananchi kusikika kuliko kutumia muda mwingi kurusha vipindio vya muziki na matangazo ya nje kama vile hapa nchini hakuna cha kutangaza.
Anmetoa wito kwa wamiliki na wakurugenzi wa vyombo vya habari kuhakikisha ghabari za vijiojini Zinapewa uzito sawa na mijini  ikizingatiwa kuwa idadi kubwa ya Watanzania ipo vijijini.
Katika Hotuba hiyo Waziri amesema kuwa Serikali za nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ziliridhia kuwa ifikapo Tarehe 31 Decemba 2012 iwe mwisho wa Analogia hivyo Watanzania wote wahakikishe wameamia katika Mfumo wa Digitali mpaka kufikia tarehe iliyo tajwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maswasiliano Tanzania Prph, John Nkoma akizungumza na waandishi wa Habari juu ya namna ya kuwahamasisha watanzania kuhamia katika mfumo wa Digitali.

Waziri pamoja na Mkurugenzi wa TCRA wakisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari

Hapa waziri akifurahia jambo kwa waandishi wa habari

Hawa ni baadhi ya wadau wamiliki na wakurugenzi wa vyombo vya habari nchini waliohudhuria katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment