Tuesday, November 6, 2012

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI KATIBU WA MUFTI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR



  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na  kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Uwanja wa Mwanakwerekwe mjini Unguja jana. Rais ambaye amerejea  leo Jumanne Novemba 6, 2012 akitokea katika ziara ya kikazi ya  juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka. Picha na Ikulu

No comments:

Post a Comment