Tuesday, October 23, 2012

AJALI MKOANI MOROGORO

 
Ajali mbaya iliyotokea maeneo ya Mikese mkoani Morogoro, roli aina Scania 113- T204 AKR likitoke Mbeya na mzigo wa viazi mviringo kuelekea Dar liliacha njia na kuanguka pembeni mwa barabara baada ya kugonga mti na kuua mtu mmoja aliekuwemo. Mashuhuda wa tukio hilo waliwaeleza wanahabari kwamba aliyekufa ni utingo wa lori hilo wakati dereva alitokomea porini baada ya ajali huku mwili wa marehemu ukipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment