Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari leo jijini Dar es salaam. |
Waziri
wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara(mwenye
koti jeupe) akisalimiana na wafanyakazi wa Wizara ya habari mara baada
ya kufungua kikao cha Baraza la wafanyakazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewataka wafanyakazi
wa wizara hiyo kutekeleza vipaumbele muhimu vya wizara ili kufanikisha
azma ya Serikali ya kuwajengea maisha bora wananchi wake.
Akifungua mkutano wa
baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam amesema
kuwa ili kufanikisha malengo na vipaumbele vilivyowekwa wizara yake
inawategemea wafanyakazi hao ambao ni nguvu kazi muhimu katika kuleta
mabadiliko ya utendaji kazi.
Amesema kuwa wizara
pamoja na mambo mengine inatekeleza masuala mbalimbali yakiwemo uandaji
wa mpango wa miaka 5 wa maendeleo ya michezo nchini, kuunda baraza la
taifa la vijana, kupatia ufumbuzi tatizo la maslahi ya wasanii na kukamilisha
mchakato wa kupata vazi la taifa.
“Ili kufanikisha utekelezaji
wa vipaumbele hivi kila mmoja wetu anawajibika kufanya kazi kwa bidii
mahali pake pa kazi bila kutegea wala kusukumwa.” Amesema Mukangara.
Amesisitiza kuwa sekta
ya michezo ikiimarishwa nchini vijana wengi watapata fursa ya kuendeleza
vipaji vyao na hatimaye kupunguza tatizo la ajira jambo ambalo
likifanyika katika tasnia ya sanaa vijana wengi wataweza kujiajiri
na kujiongezea kipato.
Naye kaimu mwenyekiti
wa Baraza hilo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa wizara ya Habari,
Vijana , Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akizungumza kwa kwa
niaba ya wajumbe wa baraza hilo amesema Baraza litatekeleza maagizo
yaliyotolewa kwa vitendo ili kuleta maendeleo ya wizara na jamii kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment