 |
Wabunge
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika
madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge
hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo
safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana
Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge
wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo
hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge
EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose
SaddrudinBhanji.
Wengine
ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo
Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi,
Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa
wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapisha pamoja na
wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na katika picha juu ni Waziri wa
Afrika Mashariki na mbunge wa Urambo Mh Samwel Sitta akiapa katika
bunge hilo jana jijini Arusha |
 |
Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake |
 |
Mh. Alhaji. Adam Kimbisa |
 |
Mhe. Anjela Charless Kizigha |
 |
Mhe Bernard Musomi Murunyana |
 |
Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi |
 |
Mh.Nderkindo Perpetua Kessy |
Mh.Charles Makongoro Nyerere
No comments:
Post a Comment