Tuesday, June 5, 2012

SUGA AFUNIKA DAR LIVE NA SAPOTI YA JUMA NATURE NA PROF JAY

Msanii mahiri wa HIP HOP ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, juzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Katika picha juu Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live
Sugu na Mkoloni wakizidi kuwadatisha mashabiki.
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.



No comments:

Post a Comment