Spika wa tatu wa Bunge jipya la Afrika Mashariki (EALA) Margaret Banbtonbg
Zziwa (49) kutoka Uganda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo uliopo
katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo. Zziwa ambaye ni Mchumi
kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora
Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za
awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote.
Zziwa (49) kutoka Uganda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo uliopo
katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo. Zziwa ambaye ni Mchumi
kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora
Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za
awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote.
WABUNGE wa bunge la Afrika mashariki
wamemchagua spika wa bunge hilo kutoka nchini Uganda ambaye ataliongoza bunge
hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Spika huyo ambaye ndio mwanamke wa
kwanza kushika wadhifa huo wa juu katika bunge hilo ni Magreth
Zziwa kutoka nchini Uganda mbaye alimbwaga mpizani wake Dora
Byamukama kwa kupata kura 33 Dora pia anatoka nchini Uganda yeye alipata kura 12.
Awali matokeo ya kura
hayakumpa Zziwa nafasi hiyo baada ya kupata kura 27 huku mpinzani
wake kura 18 na kufanya uchaguzi huo kurudiwa upya.
Aidha Mwanamama huyo ataliongoza bunge
hilo kuanzia sasa ni msomi mchumi mwenye shahada ya uzamili wa sayansi ya
siasa na uchumi.
Mara baada kuchaguliwa Spika huyo
aliapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge hilo ambapo baada ya kula kiapo
aliwashukuru wabunge wa bunge hilo kwa kumchagua.
“Naishukuru serikali yangu ya Uganda
na pia wananchi wa Uganda na ninyi wabunge kwa kunichagua kushika wadhifa huu
nawaomba ushirikiano tuendleze jumuiya yetu”alisema Zziwa.
Mara baada ya zoezi hilo wabunge 45
wa jumuiya waliapishwa rasmi kuwa wabunge wa bunge hilo kwa kipindi cha miaka
mitano ijayo.
Uchaguzi huo wa spika wa bunge hilo
ulihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za afraka mashariki na baadhi ya ndugu
waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo kwa njia ya luninga zilizofungwa nje
ya ukumbi wa bunge hilo walipongeza namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.
Bunge hilo ambalo linazinduliwa kwa
mara ya tatu na kuongozwa na Maspika kutoka nchi wanachama ambao
huchaguliwa kwa kupokezana lilianza mwaka 2001 ambapo liliongozwa na Spika
kutoka Tanzani Abdulrahaman Kinana kabla ya kupokelewa na Mkenya anayemaliza
muda wake Abdrahin Abdi.
Kazi kubwa ya bunge la Afrika Mashariki
ni kusimamia na kutunga sheria mbalimbali za uendeshaji wa mambo katika
jumuiya hiyo iliyo mbioni kuwa shirikisho la Afrika mashariki.
No comments:
Post a Comment