Stars
yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege
iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo
ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo)
itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa
11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.
Licha
ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho
(Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho
kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi
hiyo.
“Tunaiheshimu
Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji
nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini
wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi
chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.
Kikosi
cha Stars kinaongozwa na nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey
Morris. Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally,
Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri
Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.
Jonas
Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward
Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan
Singano, Simon Msuva na John Bocco.
Mbali
ya Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma
Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma
Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
Msafara
wa Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment