Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd
Shein akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini
kuhusiana na Vurugu Zilizotokezea Zanzibar,hapo katika ukumbi wa Ikulu
Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya
Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed
Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya
kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya
vurugu.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar jana,Dk. Shein
alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote,atakayethubutu kuchezea
tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”
Rais
Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita
na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa
miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali
ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya
uvumilivu wa kidini.
“Kwa
masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja
amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue
kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema Rais Dk. Shein.
No comments:
Post a Comment