Kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo
mbalimbali katika maisha,leo benki ya NMB imezindua promosheni
iitwayo jenga maisha yako na NMB itakayomwezesha mteja wake kuingia
kwenye droo na kushinda tani ya saruji, mabati ya kuwezeka,
amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB, Mkuu wa idara
ya Masoko na Mawasiliano Bw. Imani Kajula kushoto katika picha amesema “wateja wengi wanaweka amana ili kutimiza malengo
mbalimbali na ndio maana, benki ya NMB imezindua promosheni ya JENGA
MAISHA YAKO NA NMB itakayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na
NMB Junior Account watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye akaunti
zao za NMB Bonus Account au NMB Junior Account kupata riba ya kuvutia
hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana kilichowekwa” .
Kupitia droo ambazo
zitachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia
leo, sio tu zitawaongezea watanzania tabia ya kujiwekea akiba lakini
pia itasaidia watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea..
Fungua NMB Bonus Account
au NMB Junior Account leo na ushinde!!!
No comments:
Post a Comment