Thursday, May 31, 2012

SUALA LA AFYA YA UZAZI SALAMA LIPEWE KIPAUMBELE MCHAKATO WA KATIBA

Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo ya kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya iliyomalizika jana kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

BAADHI YA WAREMBO WATAKAOPANDA JUKWAANI KATIKA SHINDANO LA MISS NYAMAGANA JIJI MWANZA LEO

Aisha.
HIZI NI BAADHI YA SURA  ZITAKAZOPANDA JUKWAANI USIKU WA LEO IJUMAA,  KATIKA SHINDANO LA  MISS NYAMAGANA 2012. KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST JIJINI MWANZA.
SHUGHULI NZIMA INASIMAMIWA NA STOPPERS ENTERTAINMENT.
BURUDANI ITATOLEWA NA LINAH, DITTO NA HAFSA KAZINJA.
MSHEHERESHAJI MKUU AU MC WA SHUGHULI NZIMA NI MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA KUNDI LA ORIGINAL KOMEDI.
Amina.
Brenda
                                                                        Cecy.

MKUTANO WA SHIRIKISHI LA NGUMI LA DUNIA IBF WAENDELEA HUKO HONOLULU MAREKANI

Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani kushoto akiwa amesimama na Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi siku ya ufunguzi wa mkutano huo tarehe 31 May, 2012.
Rais Peoplers aliwakaribisha wajumbe na kuwasomea taarifa ya mwaka ya IBF/USBA ambapo zaidi ya mapambano ya ubingwa 349 yalifanyika chini ya IBF/USBA mwaka jana. 
 
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha mwakilishi wa IBF katika bara la Ulaya Roberto Reya wa Italia naye alihutubia mkutano huo.
 
Katika mkutano huo taarifa ya kifo cha bondia wa Thailkand Thangthong Kiattaweesuk aliyekuwa na miaka 35 kilitolewa rasmi. Bondia Kiattaweesuk alikufa katika ajali ya gari akiwa na mkewe, mtoto mmoja na ndugu yake baada tu ya kushinda pambano lililompa nafasi ya kupigana na bingwa wa IBF wa dunia katika uzito wa Feather Geoffrey Mathebula wa Afrika ya Kusini.
 
Kiattaweesuk alimpiga bondia wa Kenya Geofrey Munica kwa KO raundi ya 10 katika pambano la kugommbea mkanda wa mabara wa IBF.
 
Pamoja na ufunguzi huo leo kutakuwa na semina ya utibabu pamoja na semina ya majaji. Mkutano huo utamalizika tarehe 2 Juni.
 
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
 

TAIFA STARS YAWASILI ABDIJAN,KIM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU

 Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu.
 
Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.
 
Licha ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.
 
“Tunaiheshimu Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.
 
Kikosi cha Stars kinaongozwa na nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris. Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso.
 
Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.
 
Mbali ya Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
 
Msafara wa Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi hiyo.

MISS MTWARA KUFANYIKA JUMAMOSI JUNI 2 MJINI MTWARA

Warembo watakaopanda jukwani kushiriki katika shindano la  kumtafuta Miss Mtwara 2012 siku ya jumamosi juni 2 katika ukumbi wa Makonde Beach mjini Mtwara, ambapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika ukumbi huo kujiweka tayari kwa ajili ya shindano hilo.
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006) siku ya jumamosi Juni2 katika ukumbi wa makonde beach
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006),Pamoja na muandaaji wa shindano Rajab Mchatta. siku ya jumamosi Juni 2 katika ukumbi wa makonde beach

NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali katika maisha,leo benki ya NMB imezindua promosheni  iitwayo jenga maisha yako na NMB itakayomwezesha mteja wake kuingia kwenye droo na kushinda tani ya saruji, mabati ya kuwezeka, amana maradufu, ada za shule, fulana za NMB pamoja na mabegi ya shule.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano Bw. Imani Kajula kushoto katika picha  amesema “wateja wengi wanaweka amana ili kutimiza malengo mbalimbali na ndio maana, benki ya NMB imezindua promosheni ya JENGA MAISHA YAKO NA NMB itakayowezesha wateja wote wa NMB Bonus Account na NMB Junior Account watakaofungua akaunti au kuongeza amana kwenye akaunti zao za NMB Bonus Account au NMB Junior Account kupata riba ya kuvutia hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha amana kilichowekwa” .
Kupitia droo ambazo zitachezeshwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo, sio tu zitawaongezea watanzania tabia ya kujiwekea akiba lakini pia itasaidia watakaoshinda kufikia malengo waliyojiwekea..
Fungua NMB Bonus Account au NMB Junior Account leo na ushinde!!!

WAZAZI WAPINGA WATOTO WAO WANAOSOMA SHULE ZA MSINGI KISING'A KUFANYISHWA KAZI MDA WA MASOMO

Wanafunzi  wa shule ya msingi Kising'a Isimani  wilaya ya Iringa  vijijini  wakiwa  wamebeba ndoo  za maji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu jana majira ya saa 9.45 asubuhi muda ambao  walipaswa  kuwepo darasani kama  walivyokutwa na mpiga  picha  wetu.                                                                                                                                                                                                             TABIA  ya uongozi  wa shule  ya msingi Kising'a Isimani  wilaya ya  Iringa kuwatumikisha kazi wanafunzi asubuhi  wakati  wa vipindi  vya masomo imepingwa  vikali na  baadhi ya  wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika  shule  hiyo na kuiomba  wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuingilia kati suala  hilo.

Wakizungumza  na mwandishi  wa habari  hizi  leo kijijini hapo wazazi hao   walisema  kuwa  uongozi  wa  shule  hiyo ya msingi Kising'a kila  siku kabla ya  watoto  kuingia madarasani  wamekuwa   wakiwatuma katika kazi  mbali mbali  ikiwemo ya  kuchota maji   kwa ajili ya ujenzi  wa nyumba ya mwalimu.

Alisema  Jonh Kalinga  kuwa  tayari  wamepata  kuulalamikia  uongozi  wa  shule  hiyo na kuukanya kacha   kuwatumikisha  watoto  hao majira  ya masomo  ila bado vitendo  hivyo  vya  wanafunzi kukatishwa  vipindi na kwenda  kufanya kazi  za  walimu vimekuwa  vikiendelea.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA WANANCHI JUU YA VURUGU ZILIZOTOKEA HIVI KARIBUNI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbalimbali  vya Habari Nchini kuhusiana na Vurugu Zilizotokezea Zanzibar,hapo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Ukiwa ni Utaratibu wake wa kuzungumza na Vyombo vya Habari kila ifikapo mwisho wa Mwezi.
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote,atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”

Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya uvumilivu wa kidini.

“Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema  Rais Dk. Shein.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA AFDB MJINI ARUSHA LEO





Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr jakaya mrisho kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya maendeleo ya afrika (AFDB) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC mjini Arusha leo.
Rais wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr.Donald kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Mjini Arusha.
Rais wa jamhuri ya Ivory Cost Dr Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Mjini Arusha.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr jakaya mrisho kikwete(kulia) kabadilishana mawazo na waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (kushoto) Wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Mjini Arusha.


Rais wa jamhuri ya Ivory Cost Dr Alassane Ouattara(kushoto)akibadilishana mawazo na raiswa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr.Donald kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano  wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) Mjini Arusha.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano  wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hutuba ya rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbu wa mikutano wa kimataifa AICC Mjini Arusha.
Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC wakati rais Jakaya kikwete akiutubia leo.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS KIKWETE NCHIN ANGORA


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda anaondoka Dar es Salaam leo mchana (Alhamisi,  Mei 31, 2012) kwenda Luanda, Angola kuhudhuria kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu Pinda anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye leo anatarajiwa kufungua mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huko Arusha.
Mara baada ya kuwasili,  leo jioni Waziri Mkuu atahudhuria kikao cha TROIKA ambacho kinajumuisha Wakuu wa Nchi kitakachofanyika Ikulu ya nchi hiyo na usiku atashiriki hafla maalum iliyoandaliwa kwa viongozi wakuu wa nchi za SADC.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za SADC ambao umepangwa kufanyika kesho (Juni Mosi, 2012), utatanguliwa na mkutano wa mawaziri unaoanza leo (Alhamisi, Mei 31, 2012) chini ya uenyekiti wa Waziri ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini nchini kesho kutwa (Jumamosi, Juni 2, 2012).

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINIANA MKATABA NA MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA IRAN.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakisainiana mkataba wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Iran, Mhe. Mohammad Reza Rahimi, wakibadilishana mkataba baada ya kusainiana mkataba huo wa makubaliano ya pamoja ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano wa nchi hizo mbili,  wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Mei 30, 2012

DROO YA TANO YA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL,YANGURUMA TENA,MWANZA WAENDELEA KUVUNA ZAWADI

Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC.
Menejwa mawasiliano wa kampun i ya bia ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu hiyo katikati ni Meneja wa bia ya bia ya Serengeti Premium Lager na kulia ni Tumainiel Malisa kutoka PWC
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Genereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na kulia ni Abdallah Hemed kutoka bodi ya mchezo ya kubahatisha.

ZUKU YAFANYA HAFLA YA KUTANGAZA UDHAMINI WA TAMASHA LA ZIFF


Mwenyekiti wa kampuni ya  Wananchi Group kampuni inayosambaza vin'gamuzi vya televisheni ya Zuku Afrika hapa nchini Bw. Ali Mufuruki akizungumza katika hafla ya kutangaza kampuni hiyo ya Zuku Kudhamini tamasha la kimataifa la  Zanzibar International Film Festivala (ZIFF) katika hafla iliyofanyika jana kwenye ufukwe wa Slipway jijini Dar  es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tamasha la ZIFF wakiwemo wanamuziki, waigizaji wadhamini na wengeni wengi.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Shilole akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyoi. jana jion
 Waigizaji wa filamu mbalimbali wakiwa wamesimama mbele wakati walipokuwa wakitambulishwa katika hafla hiyo na mwenyekiti wa ZIFF Bw. Mahmoud Thabit Kombo.
 Kutoka kulia ni Jacob Steven. Raymond Kigosi na Cloud waigizaji wa filamu za Bongomovie wakiwa katika hafla hiyo
Mwigizaji Aunt Ezekiel kushoto akiwa na waigizaji wenzake.
 Mwigizaji Jaquiline Walper kushoto akiwa na waigizaji wengine katika hafla hiyo wa tatu kutoka kulia ni mchezaji wa timu ya Simba Uhuru Selemani.
Mwenyekiti wa ZIFF Bw. Mahmoud Thabit Kombo akiwatambulisha waigizaji pamoja na wasanii mbalimbali katika hafla hiyo jana.